a. Kutoa huduma za masomo na mafunzo katika misingi, taratibu na mbinu za kufanya kazi za Sanaa, mawasiliano ya umma na
fani nyingine zozote zinazohusiana nazo.
b. Kuwasaidia watoto, vijana na watu wazima kutimiza ndoto zao katika Sanaa ikiwemo kuwaunganisha na wasanii maarufu na
wadau wa maendeleo ya Sanaa.
c. Kutoa huduma za ushauri elekezi zinazohusiana na Sanaa na Utamaduni kwa jamii, Serikali, watu binafsi, na mashirika ya
ndani na nje ya nchi.
d. Kusaidia vijana wenye vipaji walio kwenye mazingira magumu, kwa kuwapa ufadhili wa masomo Chuoni.
e. Kuhimiza na kukuza moyo wa uzalendo na uadilifu ili wahitimu waheshimu, walinde na waenzi tunu za Taifa zikiwemo maadili,
umoja, amani na mshikamano.
f. Kukuza uelewa wa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kuandaa na kuendesha mashindano,
matamasha na maonesho ya Sanaa.
g. Kujihusisha na shughuli nyingine zozote za kielimu na kisanii kadiri Chuo kitakavyoona inafaa