Kikundi cha Ngoma za Asili na Kudansi/Keorografia
Chuo kina kikundi cha ngoma za asili kinachocheza kwa ubora ngoma halisi (zisizotiwa vionjo vya kisasa) za makabila mbalimbali
ya Tanzania, ambacho kinafanya maonesho kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali. Pia tuna kikundi cha wachezaji
muziki na keorografia. Vikundi hivi vinafanya maonesho kwa gharama nafuu lakini kwa ubora mkubwa. Tunawaalika wadau
mbalimbali kuvitumia vikundi hivi kwenye shughuli mbalimbali za kitamaduni na burudani.