Mafunzo
Chuo kinatoa mafunzo ya aina mbili:
- a. Mafunzo ya Kitaasisi
Ni mafunzo ya kawaida yaliyozoeleka yanayotolewa katika mazingira rasmi ya Chuoni, kupitia mihadhara ya darasani na
semina kwa kutumia vifaa maalum vya kufundishia.
Ambayo huambatana na mazoezi ya vitendo kwenye maabara, karakana, saluni na studio za Chuo; pamoja na mazoezi ya vitendo na mafunzo ya vitendo uwandani.
-
b. Mafunzo ya Uanagenzi
Ni mafunzo ya vitendo yanayofanyika moja kwa moja kwenye maabara, karakana, saluni au studio maarufu za mtaani ambapo wanachuo hujifunza kwa kushirikiana na wasanii maarufu au wafanyakazi wenye uzoefu.
Uanagenzi unalenga kuwapa wanachuo ujuzi wa moja kwa moja na uzoefu wa kazi halisi ya Sanaa.