Elimu ya Ugani
Chuo cha Sanaa Dar es Salaam kinatoa Mafunzo ya Ugani, nje ya Chuo na hasa mikoani, kwa ajili ya kuendeleza maarifa, ujuzi,
ustadi, mbinu mpya, na mawasiliano na mahusiano kwa watu waliopo nje ya mfumo rasmi wa elimu au wasioweza kuufikia mfumo
rasmi wa elimu, kwa lengo la kuwawezesha kujifunza, kukuza vipaji vyao, kurasimisha ujuzi wao na kuwatunuku vyeti. Mafunzo
hutolewa kwa njia za semina, maonyesho, na mtandaoni. Wasiliana nasi kujua ratiba ya Mafunzo ya Ugani karibu yako