Studio hii pamoja na kutayarisha bure kazi za wanachuo, inatoa huduma kwa gharama nafuu kwa wasanii mbalimbali wa nje na
jamii kwa ujumla. Tunatoa huduma za upigaji wa picha za video kwenye matukio mbalimbali, uzalishaji wa muziki, ubunifu wa
sauti na uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni.