CHUO CHA SANAA DAR ES SALAAM


"Kipaji ni Ajira. Sanaa ni Biashara"

KANUSHO LA TOVUTI YA CHUO

KANUSHO LA TOVUTI YA CHUO CHA SANAA DAR ES SALAAM

Tovuti hii (Chuo cha Sanaa Dar es Salaam), inayomilikiwa na CHUO CHA SANAA DAR ES SALAAM, imetengenezwa kwa madhumuni ya kutoa taarifa kuhusu Chuo, kozi zinazotolewa, matukio, shughuli zingine za Chuo, na mambo mengine yanayohusiana na masuala ya Sanaa, Utamaduni na Elimu. Kwa kutumia tovuti hii, unakubaliana na masharti na vigezo vilivyoainishwa katika Kanusho hili.

1. Usahihi wa Taarifa

Tunajitahidi kuhakikisha kuwa maudhui yaliyomo kwenye tovuti hii ni sahihi na ya hivi karibuni. Hata hivyo, hatutoi uhakikisho wowote kuhusu ukamilifu, usahihi, au uhalali wa taarifa hizo. Chuo hakitawajibika kwa makosa yoyote au upungufu wowote unaoweza kutokea katika maudhui yaliyopo.

2. Hakimiliki na Haki Miliki

Maudhui yote yaliyomo kwenye tovuti hii, yakiwemo maandishi, picha, nembo, na nyaraka nyingine, yanamilikiwa na Chuo cha Sanaa Dar es Salaam, isipokuwa pale inapobainishwa vinginevyo. Tafadhali soma na zingatia Mwongozo wa Haki Miliki ya Tovuti hii.

3. Ushauri wa Kitaalamu

Taarifa zinazotolewa kwenye tovuti hii ni kwa madhumuni ya jumla na hazipaswi kuchukuliwa kama ushauri wa kitaalamu, ikiwa ni pamoja na ushauri wa masuala ya elimu, kifedha, au sheria. Tunashauri wageni wa tovuti kutafuta msaada wa kitaalamu inapohitajika.

4. Viungo Muhimu

Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti zingine kwa madhumuni ya taarifa zaidi. Hata hivyo, Chuo cha Sanaa Dar es Salaam hakihusiki na maudhui au Sera za Faragha za tovuti hizo, na hatutawajibika kwa madhara yoyote yanayotokana na matumizi ya viungo hivyo.

5. Dhima

Chuo cha Sanaa Dar es Salaam hakitawajibika kwa hasara yoyote, iwe ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, inayoweza kusababishwa na matumizi ya tovuti hii, ikiwa ni pamoja na upotevu wa data, mapato, au madhara mengine yanayotokana na matumizi ya taarifa zilizopo kwenye tovuti hii.

6. Mabadiliko ya Kanusho

Chuo cha Sanaa Dar es Salaam kina haki ya kufanya marekebisho ya maudhui ya tovuti hii, ikiwa ni pamoja na Kanusho hili, wakati wowote bila kutoa taarifa ya awali. Tunashauri wageni wa tovuti yetu kuangalia ukurasa huu mara kwa mara ili kupata taarifa za hivi karibuni. Kwa kutumia tovuti hii, unakubali masharti yote yaliyomo kwenye Kanusho hili.

Ikiwa una maswali au maoni kuhusu tovuti hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

  • Chuo cha Sanaa Dar es Salaam
  • 1176 Mt. Kibamba St. 16110 Kibamba, Kando ya Barabara ya Morogoro.

    S.L.P 72115, Dar es Salaam, Tanzania.

  • +255 715 910 010
  • karibu@dararts.ac.tz