CHUO CHA SANAA DAR ES SALAAM


"Kipaji ni Ajira. Sanaa ni Biashara"

SHULE YA UREMBO

SHULE YA UREMBO

Shule ya Urembo ni kitengo maalum cha mafunzo ya Cosmetology chini ya Chuo cha Sanaa Dar es Salaam, kinachotoa mafunzo ya nadharia na vitendo katika masuala ya urembo, huku kikitoa huduma kwa jamii kama sehemu ya mazoezi ya vitendo ya wanachuo.

Shule hii inalenga:

  • • Wanawake na wanaume wanaotaka kujifunza fani za urembo kitaalamu.
  • • Wanajamii wanaohitaji huduma za salon kwa gharama nafuu.
  • • Wanachuo wanaosomea Cosmetology kwa ajili ya mazoezi zaidi ya vitendo.

Tunatoa: 1. Mafunzo ya Cosmetology (Nadharia na Vitendo)

  • • Kusuka na kufunga nywele
  • • Kuosha nywele
  • • Kutibu nywele
  • • Kuosha, kutibu na kurekebisha wig
  • • Kupunguza nywele na kuzistaili
  • • Makeup (kawaida na maalum)
  • • Manicure na Pedicure (Utunzaji wa kucha na ngozi za mikono na nyayo).
  • • Ushauri wa ngozi na vipodozi
2. Huduma za ubora za Salon kwa Wanawake, zikiwemo:
  • • Kusuka na kufunga nywele
  • • Kuosha nywele
  • • Kuosha, kutibu na kurekebisha wig
  • • Kutibu nywele
  • • Kupunguza nywele na kuzistaili
  • • Makeup (kawaida na maalum)
  • • Manicure na Pedicure
  • • Ushauri wa msingi wa ngozi na vipodozi (bure)

Mahali Tulipo Shule ya Urembo ipo ndani ya majengo ya Chuo cha Sanaa Dar es Salaam, katika upande wa nje wa barabara ya mtaa, hivyo kuwarahisishia wanajamii kufika bila kuingia katika majengo ya utawala na madarasa.

Muda wa Huduma Huduma za salon kwa wanajamii hutolewa kila siku, kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 usiku (ikiwemo siku za wikiendi na mapumziko).

Umuhimu wa Shule ya Urembo

  • • Kutoa mafunzo ya vitendo yanayolingana na mahitaji halisi ya soko.
  • • Kuwezesha wanachuo kupata uzoefu wa kazi halisi kabla ya kuhitimu.
  • • Kutoa huduma bora za urembo kwa wanachuo, wafanyakazi, na jamii kwa gharama nafuu.

Zingatia

  • • Mafunzo yanaendeshwa kwa kutumia miongozo na mitaala rasmi ya Chuo.
  • • Nadharia hufundishwa katika madarasa ya Chuo, na vitendo hufanyika ndani ya salon.
  • • Huduma zote hutolewa kwa kuzingatia usafi, usalama wa afya, maadili ya kitaaluma, na usimamizi wa wakufunzi wabobevu.

Jiunge nasi leo na anza safari yako ya taaluma ya urembo. (Bonyeza hapa kujaza fomu ya kujiunga na kozi)