Kila mtu anacho kipaji chake fulani. Sisi tunajikita katika vipaji vya Sanaa; kuviibua, kuvikuza,
na kuviendeleza kuwa ujuzi wa kitaalamu. Moja ya maswali yanayoibuka mara kwa mara ni: 'Je,
kusomea Sanaa kuna uhakika wa ajira?' Jibu ni NDIYO KUNA UHAKIKA WA AJIRA.
Tunakuhakikishia kuwa Sanaa ni lango la fursa; kupitia vipaji vyao, wahitimu wetu wanaweza
kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi, ikiwemo utumishi wa umma kama vile majeshi ya Ulinzi
na Usalama.
Chuo cha Sanaa Dar es Salaam huandaa wahitimu kwa maarifa na ujuzi wa hali ya juu,
kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kujitegemea au kushindana katika soko la ajira la ndani
na nje ya nchi kwa ufanisi. Na ndiyo maana tunathibitisha kuwa kupitia Chuo chetu kuwa na
Kipaji ni Ajira!