Sanaa si burudani tu, bali ni biashara rasmi, yenye thamani na inayotambulika kisheria.
Tunawaandaa wahitimu wetu kuwa si tu wasanii bora, bali pia wafanyabiashara mahiri katika
sekta ya Sanaa. Kupitia kozi yetu ya Usimamizi wa Sanaa, tunawafundisha jinsi ya kubadilisha
Sanaa zao kuwa biashara rasmi na endelevu kwa kuzingatia misingi ya masoko, fedha, na
ujasiriamali.
Tunawasaidia kujenga majukwaa rasmi ya kisheria, kuandaa mikakati ya biashara, na
kuwaunganisha na fursa za kitaifa na kimataifa. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi zao za
Sanaa zinawaletea mapato stahiki na kuwaweka katika nafasi ya kuthaminiwa kama
wafanyabiashara wengine.
Chuo cha Sanaa Dar es Salaam kinawandaa si tu kuwa wasanii, bali pia kuwa wajasiriamali
wenye mafanikio katika sekta ya Sanaa. Kwasababu hapa kwetu Sanaa ni Biashara yenye
thamani!