Chuo cha Sanaa Dar es Salaam ni taasisi ya kisasa inayoongoza nchini Tanzania katika kutoa
mafunzo ya kina ya Sanaa za kitamaduni na za kisasa. Tunazingatia mbinu za kisasa za
ufundishaji, na kuweka msisitizo mkubwa kwenye mazoezi ya vitendo ili kuhakikisha kila
mwanachuo; bila kujali umri, hali, nafasi, kipato, au elimu, anakuwa mahiri katika fani yake ya
Sanaa aliyoichagua.
Hapa Chuoni, tunaamini kuwa kila ndoto ya mwanachuo ina thamani. Ndiyo maana tunaweka
na kutekeleza mikakati maalum kuhakikisha kila mwanachuo, zaidi ya kupokea mafunzo bora,
anapata msaada wa kitaalamu ili kufanikisha ndoto yake ya Sanaa.
Maisha ya chuoni ni mchanganyiko wa taaluma na burudani. Wanachuo wetu husoma huku
wakijiongezea kipato kupitia kazi za Sanaa wanazotengeneza wenyewe, wakipata fursa za
kuonesha vipaji vyao kwenye matamasha makubwa na vituo vya televisheni. Chuo pia
kinawaunganisha moja kwa moja na wasanii maarufu pamoja na taasisi zinazojihusisha na
sekta ya Sanaa, hivyo kuwapa mtandao wa fursa kwa maendeleo yao ya kitaaluma na kiuchumi.