Chuo cha Sanaa Dar es Salaam kinawahakikishia wote wenye uhitaji wa kusoma Sanaa, lakini
wanakosa nafasi ya kutosha kuhudhuria vyuoni, kwamba hapa tuna nafasi zinazowawezesha
kusoma bila ya kuathiri majukumu yao mengine. Hayo yanawezekana kutokana na:
Muundo wa Kozi
Tuna kozi ndefu za miezi kumi na miwili (12) na kozi fupi za miezi mitatu (3).
Zamu za Kusoma
Tuna zamu za aina nne kwa siku, ambapo mwanachuo huchagua zamu moja kulingana na
nafasi yake. Zamu hizo ni Zamu ya Asubuhi, Zamu ya Jioni, Zamu za Muda Mfupi na
Madarasa ya Nyumbani/Ofisini.
Mafunzo ya Uanagenzi
Ni mafunzo ya vitendo yanayofanyika moja kwa moja kwenye maabara, karakana, saluni au
studio maarufu za mtaani ambapo wanachuo hujifunza kwa kushirikiana na wasanii maarufu au
wafanyakazi wenye uzoefu. Wanachuo hawahudhurii madarasani Chuoni.
Mafunzo ya Ugani
Mafunzo ya Ugani hufanyika nje ya Chuo, hasa mikoani, kwa ajili ya kuendeleza maarifa, ujuzi,
ustadi, mbinu mpya, na mawasiliano na mahusiano kwa wasanii au wenye ndoto za kuwa
wasanii waliopo nje ya mfumo rasmi wa elimu au wasioweza kuufikia mfumo rasmi wa elimu,
kwa lengo la kuwawezesha kujifunza, kukuza vipaji vyao, kurasimisha ujuzi wao na kuwatunuku
vyeti.